Papa Francis awateua makadinali 17 wapya

Papa Francis amewateua makadinali 17 wapya
Image caption Papa Francis amewateua makadinali 17 wapya

Papa Francis amewachagua makadinali 17 wapya.

Kumi na tatu kati yao ni wa umri wa chini ya miaka 80, na hivyo wataweza kupiga kura kumchagua papa mpya itakapohitajika.

Papa Francis anaendelea kujaribu kuingiza wawakilisha kutoka sehemu mbali mbali za dunia katika Kanisa Katoliki.

Wengi kati ya makadinali wapya ni kutoka nchi zinazoendelea.

Watashika nyadhifa zao mwezi ujao.