Juan Manuel kutoa fedha za Nobel kusaidia wahanga

Juan Manuel Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais wa Colombia Juan Manuel atoa fedha za nishani yake kusaidia wahanga

Rais wa Colombia na mshindi wa Nobel , Juan Manuel Santos amesema atachangia fedha kutokana na nishani yake amani ili kusaidia wahanga wa machafuko nchini humo.

Santos alishinda nishani hiyo ikiwa ni matokeo ya jitihada zake katika kufikia makubaliano ya Amani na kundi la wapiganaji la FARC yajulikanayo kama Timochenko.

Makubaliano hayo yalisainiwa mwezi uliopita kumaliza mapigano yaliyodumu kwa zaidi ya miongo mitano.

Santos anatarajia kukabidhiwa Zaidi ya dola 9000 kutoka kwa kamati ya tuzo ya Nobel mji mkuu Norway, Oslo.