Uchunguzi wa kifo cha Hughes unaanza baada leo

Hughes Haki miliki ya picha Google
Image caption Philip Hughes

uchunguzi unaanza baadae hii leo huko Australia juu ya kifo cha mcheza Kriketi Philip Hughes. mchezaji huyu alifariki miaka miwili iliyopita baada ya kupigwa na mpira shingoni wakati wa mchezo huko Sydney.

Jeraha hilo lilisababisha ubongo kuchanganyika na damu na kumsabishia kifo siku mbili baadae.Wachunguzi watachunguza kama kulikua na uwezekano wa kutumia kifaa kingine cha kuuokoa maisha ya mchezaji huo.

Mapema mwaka huu tathmini huru imeonesha kuwa kutumia kofia ngumu na ya kisasa ingeweza kuzuia ajali hiyo iliyopelekea kifo cha mchezaji huyo