Mchuuzi anayevalia nadhifu Zimbabwe
Huwezi kusikiliza tena

Mchuuzi anayevalia nadhifu Zimbabwe avutia wateja

Kuna zaidi ya wachuuzi 100 000 katika barabara za mji mkuu wa Zimbabwe, Harare. Lakini mmoja kati yake ni tofauti.

Farai Mushayademo, ni mwuzaji maji, na bila shaka ndiye mchuuzi anayevalia nadhifu zaidi miongoni mwa wachuuzi hao.

Yeye huuza maji na bidhaa nyingine kwa wenye magari katikati mwa mji wa Harare, kila wakati akiwa amevalia nadhifu.