Blaise Compaore aonekana hadharani mara ya kwanza

Blaise Compaore (kulia)
Image caption Blaise Compaore (kulia)

Aliyekuwa rais wa Burkina Faso aliyepinduliwa mwezi Oktoba mwaka 2014 Blaise Compaore, ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu alazimishwe kukimbilia uhamishoni katika taifa jirani la Ivory Coast.

Bwana Compaore alimtembea aliyekuwa rais wa Ivory Coast Henri Konan Bedie mjini Abidjan lakini hakusema chochote na vyombo vya habari.

Mwandishi wa BBC alichukua picha ya bwana Compaore akishikana mikono na bwana Berdie.

Wadadisi wanasema kuwa rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara ana deni la bwana Compaore kwa kuongoza mapatano yaliyomaliza mzozo nchini mwake na hivyo hana mipango ya kumrudisha Burkina Faso.