Ethiopia yazilaumu Misri na Eritrea kwa kuchangia ghasia nchini mwake

Vikosi vya usalama vimelaumiwa kwa kutumia nguvu nyingi dhidi ya waandamanaji Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Vikosi vya usalama vimelaumiwa kwa kutumia nguvu nyingi dhidi ya waandamanaji

Wazizi wa habari nchini Ethiopia anasema kuwa makundi nchini Eritrea na Misri yanachangia kuwepo ghasia ambazo zimesababisha kutangazwa hali ya harati ya miezi sita nchini humo.

Getachew Reda alisema kuwa vikundi vinawapa silaha na pesa makundi ya upinzanani. Chini ya hatua ya kutangaza hali ya hatati wanajeshi watatumwa kuzima maandamano.

Hii inafuatia miezu kadha ya maandamano ya kuipinga serikali yanayofanywa na makabil mawili makubwa zaidi nchini humo

Ghasia zimeongezeka tangua mwanzo wa mwezi huu wakati takriban watu 55 waliuawa wakati wa maandamano kwenye warsha moja ya dini ya kabila la Oromo.

Waziri huyo pia aliilaumu Eritrea ambayo Ethiopia imekuwa na mzozo wa mpaka nayo kwa muda mrefu.

Ethiopia pia imekuwa na tofauti na Misri baada ya uamuzi wa Ethiopia wa kujenga bwawa kwenye mto Nile