Utafiti: Wanawake wengi 2016 wanafurahia kuwa wanawake

mwanmke ajitizama kwenye kioo katika miaka ya 1940 Haki miliki ya picha Thinkstock

Karibu wanawake 9 kati ya 10 wanaridhia kuwa mwanamke kuliko mwanamume leo, ikilinganishwa na nusu ya idadi ya leo katika miaka ya 1940, utafiti wa BBC umedhihirisha.

Utafiti huo pia umedhihirisha wanawake mwaka 2016 wanafurahia ndoa.

Asilimia 42 wanasema wanawake na wanaume wamejitolea kiwango sawa cha uhuru wao katika ndoa.

Ni robo moja ya wanawake na wanaume walioshirika katika utafiti 1951 walihisi hivyo.

Watafiti waliozungumza na wanawake 1,004 wa miaka tofauti walichunguza maisha yao na kubadilika kwa mienendo, katika masuala ya ndoa, pesa, ngono, familia kazi na muonekano. Haya ndio matokeo.

Ndoa

Haki miliki ya picha Thinkstock

Wanawake wa leo huenda wakataka kuolewa na mwanamume walie naye sasa tofuati na wanawake wa miaka ya 1940.

Kati ya wanawake waliofanyiwa uchunguzi 87% wanasema watasalia na waume zao, katika miaka ya 1949 utafiti wa wanawake na wanaume ulidhihirisha kuwa 77% wangebadilisha wana ndoa wao iwapo wangepata nafasi.

Mwanamke mmoja kati ya 10 huedna wangeolewa na mtu tofauti kwa mujibu wa utafiti huo wa kipindi cha Woman's Hour BBC.

Kazi

Haki miliki ya picha Thinkstock

Wanawake wa umri tofauti huedna wanafanya zaidi leo ikilinganishwa na 1951 - 60% ya wanawake wameajiriwa leo ikilinganishwa na 31% miaka 65 iliopita.

Tofauti ni kubwa zaidi kwa wanawake wa umri mkubwa - leo ni 62% ya wanawake wa umri wa kati ya 55 hadi 64 wanaofanya kazi ikilinganishwa na 22% mnamo 1951.

Walipoulizwa ni kwanini wameamua kufanya kazi, zaidi ya nusu ya wanawake walio na umri wa kati ya miaka 18 na 64 wamesema sababu kuu ni kujiheshimu, ikifuatwana pesa, alafu wenzao na pia mazingira ya kufanya kazi.

Wanawake wa umri wa miaka 65 na zaidi huedna wangetaja pesa ikilinganishwa na sababu nyengine, utafiti umeashiria.

Pesa

Haki miliki ya picha Thinkstock

umusi ya wanawake wote waliochunguzwa wanasema masuala ya pesa ndio tatizo la dharura linalowakabili na familia zao, na ni jambo lililo na shinikizo kubwa kwa walio na umri wa miaka 25 hadi 34 (28%).

Muonekano

Haki miliki ya picha Thinkstock

Muonekano ni jambo lililowagusa zaidi walio na umri wa miaka 18 hadi 24, waliosema hawangependa kuitwa wanono (37%).

Wanasema hawangependa kuitwa "wajinga" na "wasiokuwa na wacheshi". (42%).

Wanawake wa umri kati ya miaka 25 na 34 huenda walifanyiwa upasuaji wa urembo (10%), wanaofikiria kufanyiwa upasuaji huo katika siku zijazo (46%) na kusema muonekano wao ni muhimu zaidi sasa kuliko walivyokuwa miaka 21 (16%).

Mapenzi

Haki miliki ya picha Thinkstock

Karibu robo ya wanawake wa kati ya umri wa miaka 25 hadi 34 wanadai "kuridhika kupita kiasi" chumbani.

Wanawake wa umri wa kati ya miaka 55 hadi 64 ndio walionekana kutoridhika kupita kiasi (16%) na ambao hawaridhiki kupita kiasi ni (9%).

Familia

Haki miliki ya picha Thinkstock

Katika suala la kuzaa, uchunguzi umedhihirisha kuwa wanawake walio na kipao cha (£40,000-na zaidi) wanafikiria mara mbili zaidi ya walio na kipato cha chini ya (£20,000) kuwa kutozaa ndio uamuzi bora.

Zaidi ya nusu ya waliochunguzwa wamehisi kuwa watoto wawili ndio idadi inayopendeza kwa familia.

Wasiwasi

Haki miliki ya picha Thinkstock

Walio na wasiwasi mkubwa ni wa umri wa kati ya 25-34 kuhusu afya yao, familia na marafiki. Afya ni (68%), kuwa na fedha za kutosha wakistaafu (53%) na kufanikisha maisha (51%).

Huenda wasijione kuwana furaha zaidi ya mama zao walipokuwa katika umri walio nao sasa.