Ureno, Ubelgiji wapata ushindi wa kishindo

Michezo tisa ya kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la dunia la mwaka 2018 imechezwa barani ulaya mataifa ya Ubelgiji,Ureno na Ufaransa yakishinda michezo yao.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wachezaji wa Ubelgiji wa wakimpongeza Axel Witsel baada ya kuifungia timu yake bao

Mashetani wekundu Ubelgiji wakicheza ugenini wamewabugiza wenyeji wao Gibraltar kwa mabao 6-0, mshambuliaji Christian Benteke, akifunga mabao matatu mabao mengine yakifungwa na Dries Mertens,Eden Hazard na Kiungo Axel Witsel.

Ureno wakawachapa kisiwa cha Faroe, kwa kichapo cha mabao 6-0 Andre Silva, akiibuka shujaa kwa kufunga mabao matatu peke yake.

Ufaransa nao wakawatambia Uholanzi nyumbani kwa kuwafunga bao 1-0 bao hilo la ushindi likifungwa na mchezaji ghali duniania Paul Pogba.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wachezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa wakipngezana baada ya Paul Pogba kufunga

Bosnia -Herzegovina, wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cyprus, Estonia wakiwa nyumbani wamekubali kulala kwa kuchapwa kwa mabao 2-0 na Ugiriki.

Latvia nao wamefungwa kwa mabao 2-0 na Hungary, Huku Andorra wakishindwa kutamba nyumbani baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 toka kwa Switzerland.

Belarus na Luxembourg wametoshana nguvu kwa sare ya goli 1-1,Sweden wametakata nyumbani kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Bulgaria