Nadal, Federer watupwa nje nne bora

Rafael Nadal na Roger Federer Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rafael Nadal na Roger Federer

Nyota wawili wa mchezo wa tenesi Rafael Nadal na Roger Federer wamekosekana kwenye nafasi nne za juu za ubora wa viwango vya mchezo wa tenesi dunia hii ikiwa ni mara ya kwanza katika muda wa miaka 13.

Kwa nyakati tofauti nyota hawa walishawahi kushika nafasi ya kwanza ya viwango vya ubora wa mchezo huu.

Rafael Nadal mwenye umri wa miaka 30 anashika nafasi ya tano huku Roger Federer akiwa katika nafasi ya saba kwa ubora.

Serbia Novak Djokovic ndie kinara akishika nafasi ya kwanza kwa ubora wa viwango vya mchezo huo duniani.

Haki miliki ya picha Google
Image caption Novak Djokovic

Orodha kamili ya wachezaji bora

1 Novak Djokovic

2 Andy Murray

3 Stan Wawrinka

4 Kei Nishikori

5 Rafael Nadal

6 Milos Raonic

7 Roger Federer

8 Gael Monfils

9 Tomas Berdych

10 Dominic Thiem