Serikali ya Colombia na waasi wa ENL kufanya mazungumzo

Colombia Haki miliki ya picha Google
Image caption Rais wa Colombia Juan Manuel Santos kufanya mazungumzo na waasi wa ENL

Serikali ya Colombia na kundi la waasi la National Liberation Army, ELN wamekubaliana kuanza mazungumzo rasmi ya amani ifikapo Oktoba 27 mwaka huu. Mazungumzo ya kwanza yanatarajiwa kufanyika makao makuu ya mji wa Ecuado,Quito.

Akizungumza kupitia Televisheni Rais Huan Manuel Santos amewahakikishia raia wa Colombia kuwa wanafikia amani ya kudumu baina yao na kundi la waasi la ELN

"Wapendwa raia wa Colombia,sisi ni taifa maalumu,linalokua kupitia mazingira magumu na ambalo linajua namna ya kubadilika kuzielekea fursa.Na hicho ndicho tutakachokwenda kukifanya sasa,kulinda amani ambayo tumeihangakia vilivyo.Haitatuponyoka katika vidole vyetu.Badala yake amani itaimarika kama ambavyo tunasonga mbele na ELN kufikia amani kamili''.Amesema Santos

Pamoja na kufikiwa kwa makubaliano hayo Rais wa Colombo Juan Manuel Santosh ametaka kuachiwa huru kwanza kwa mateka wote wanaoshikiliwa waasi hao.

Waasi hao bado wanawashikilia watu kadhaa,ambapo wamewaachia mateka watatu tu ndani ya wiki mbili zilizopita.

Kati ya wanaoshikiliwa yupo mwanasiasa maarufu Odin Sanchez ambaye mwezi April mwaka huu alijikabidhi kwa hiari yake mikononi mwa waasi kwa lengo la kumkomboa kaka yake Gavana wa zamani wa jimbo la Choco.

Kundi la waasi la ELN ni la pili kwa ukubwa nchini humo lenye wapiganaji 1500,na ambalo kwa kipindi kirefu limekuwa likijipatia fedha zake kutokana na utekaji na malipo ya fidia.