Mzigo wa ndoa za utotoni Tanzania

mischana anaosma

Tanzania na Burundi ni miongoni mwa mataifa yalioorodheshwa kuwa maeneo mabaya kuwa msichana.

Umaskini ukiwa ndio chanzo kikuu.

Utafiti wa Shirika la kimataifa la kutetea haki za watoto, Save the Children umeonyesha kuwa sheria za kitamaduni zinaruhusu makabila kufuata na kufanya maamuzi kulingana na itikadi na tamaduni za makabila hayo.

Ndoa za watoto zimewaathiri wasichana wengi duniani, na zimeanza kupungua tu katika miaka ya hivi karibuni.

Serikali ya Tanzania iliwasilisha ombi la kukata rufaa uamuzi wa kihistoria nchini uliopinga ndoa za watoto walio chini ya umri wa miaka 18.

Mnamo mwezi Julai mahakama kuu iliamua kuwa sehemu za sheria ya ndoa mwaka 1971, iliyoruhusu wasichana kuolewa wakiwa na umri wa hata miaka 14 ni kinyume na katiba.

Hatahivyo mzigo wa tatizo hili haukugawanyika sawa miongoni mwa mataifa.

Wasichana kutoka baadhi ya jamii huenda wakaolewa mapema kushinda jamii nyengine katika mataifa mbalimbali duniani.

Tanzania kwa mfano, wasichana kutoka familia maskini huenda wamo katika hatari ya kuolewa mapema mara nne zaidi ya wasichana wanaotoka familia tajiri, inasema ripoti ya Save the Children.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa 37% ya wanawake Tanzania walio na umri wa kati ya miaka 20 hadi 24 waliolewa kabla ya kutimia miaka 18.

Katika maeneo ya mashinani, baadhi ya wasichana huolewa wakiwa na hata miaka 11.

Wanandoa watoto

Msichana 1 chini ya miaka15

huolewa "kila

sekundi 7

duniani"

Carolina Thwaites

Tanzania pia ni miongoni mwa nchi zinazotajwa kushuhudia viwango vikubwa vya mimba za wasichana wadogo duniani.

Save the Children linapendekeza kuwa ni muhimu kuhakikisha sera zilizoidhinishwa katika mataifa hayo ya Afrika mashariki zinatekelezwa kulinda haki za wasichana.