Tani 20 za madawa ya kulevya zakamatwa na polisi wa Uhispania

Wachanganuzi wanaamini kuwa madawa hayo yalikuwa yametumiwa kununua silaha. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wachanganuzi wanaamini kuwa madawa hayo yalikuwa yametumiwa kununua silaha.

Mashua iliyokuwa imebeba karibu tani 20 za madawa ya kulevya ya hashish iliyokuwa safarini kwenda nchini Libya ikitokea Uturuki imekamatwa na polisi wa Uhispania kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Wachanganuzi wanaamini kuwa madawa hayo yalikuwa yametumiwa kununua silaha.

Kikosi hicho ni sehemu ya oparesheni ya kimataifa ambayo imeshika mashua mbili zilizokuwa zikisafirisha bunduki na nyingine tano zilizokuwa zimebeba madawa ya hashish.

Kwa ujumla mashua tano zimeshikwa zikiwa na bunduki 11,400 na tani 10 ya kemikali ya ammonium nitrate ambayo inaweza kutumiwa kutengeneza mabomu.

AFP inasema haijulikani madawa hayo yalikuwa yanapelekwa wapi lakini mji wa Misrata ni nyumbani kwa makundi ya wanamgambo na ni miongoni mwa wale waliouteka mji mkuu Tripoli mwaka 2014.