Ujerumani,Norway zashinda

Timu tisa za barani ulaya zilishuka katika viwanja tisa kusaka alama tatu muhimu za kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la dunia zitazofanyika nchini Urusi mwaka 2018.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mfungaji wa bao la kwanza la Ujerumani Julian Draxler

Michezo ya kundi C Ujerumani wakicheza nyumbani wamepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ireland ya Kaskazini mabao ya timu hiyo yakifungwa na mshambuliaji Julian Draxler na kiungo Sami Khedira.

Norway wakitumia uwanja wa nyumbani wa Ullevaal wameibuka na ushindi wa kishindo kwa kuichapa San Marino kwa mabao 4-0, Jamuhuri ya Czech wametoshana nguvu kwa sare ya bila kufungana na Azerbaijan.

Kundi E Poland wamewatambia Armenia kwa kuwachapa kwa mabao 2-1, Denmark wamekubali kulala kwa bao 1-0 nyumbani dhidi ya Montenegro, Kazakhstan na Romania wametoka sare ya bila kufungana.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Golikipa wa England Joe Hart akiokoa mchomo uliokua unaelekea nyavuni

Kundi F England wakicheza ugenini katika dimba la Stozice, wamekwenda sare ya bila kufungana na wenyeji wao Slovenia. Slovakia wameifunga Scotland kwa mabao 3-0.Lithium nao wameshinda nyumbani kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Malta