Steve Bruce kuwa kocha mpya wa Aston Villa

Steve Bruce Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Steve Bruce anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha mpya wa Aston Villa

Klabu ya soka ya Aston Villa ya England inatarajiwa kumtangaza Steve Bruce kuwa meneja mpya wa timu hiyo leo jumatano baada ya kumtimu kocha wake Roberto di Matteo.

Bruce mwenye umri wa miaka 55 alikua kocha wa Hull City, kabla ya kubwaga manyaga mwezi Julai mwaka huu.

Mmiliki na mwenyekiti wa Aston Villa, Dr Tony Xia, ameandika katika mtandao wa Twita, kuwa kocha huyo atatambulishwa na ni wakati wa kuwa pamoja na kuirejesha timu katika sehemu nzuri.

Villa wako katika nafasi ya 19 katika ligi daraja la kwanza (Champinship).Bruce amewahi kuvinoa vilabu vya Birmingham City, Wigan Athletic na Sunderland.