Rais Obama amesema Trump hafai kuwa rais

Donald Trump
Image caption Mgombea Urais nchini Marekani Donald Trump

Rais wa Marekani Barak Obama amewataka wanasiasa wa Republican kujiondoa rasmi kumuunga mkono Donald Trump kama mgombea wao,kwa madai kuwa hafai.

Katika mkutano wa hadhara na wafuasi wa Hillary Clinton, Obama amesema kuwa haina maana kukemea hotuba tata ya Trump kuhusu wanawake, huku wakiendelea kumuunga mkono katika nafasi ya Urais, na kudai kuwa hiyo haina maana kwake.

Viongozi wakubwa wa Republican akiwemo msemaji wa chama hicho, Paul Ryan wamejiweka mbali na Donald Trump baada ya kuwekwa hadharani video inayomuonesha Trump akiwakashifu wanawake.Hatua hiyo imekuja huku asilimia 10 ya viongozi wa chama cha Republican wakimtaka Trump kujiondoa katika kinyang'anyiro hicho .

Trump alimjibu Ryan,kuwa kwa matammshi hayo ameonyesha kuwa yeye ni kiongozi dhaifu ,amesisitiza kwamba amejipanga kuipigania Marekani kwa njia anayoona inafaa.