Kim Kardashian West ashtaki kwa kudaiwa 'kuigiza wizi'

Kim Kardashian West (maktaba) Haki miliki ya picha AP
Image caption Kim Kardashian West aliibiwa na watu waliovalia kama maafisa wa polisi mjini Paris

Nyota wa ugizaji wa televisheni wa maisha ya uhalisia Kim Kardashian West ameshtaki tovuti moja ya udaku kuhusu wasanii kwa kudai kwamba aliigiza kisa cha wizi mjini Paris wiki iliyopita.

Kwenye kesi hiyo, anataka alipwe kiasi cha pesa ambacho hakijafichuliwa kwa kuharibiwa jina.

Ameshtaki tovuti ya MediaTakeout, pamoja na mwanzilishi wake, Fred Mwangaguhunga.

Nyota huyo alifungwa mikono na majambazi waliokuwa na bunduki ambao waliingia kwenye chumba chake hotelini Paris mapema mwezi huu, polisi wanasema.

Wezi hao walitoroka na vito vya jumla ya $10m (£8m).

Kwenye kesi hiyo iliyowasilishwa mahakamani New York, anasema baada ya kuwa "mwathiriwa wa kisa cha kuogofya cha wizi wa kutumia silaha Ufaransa, Kim Kardashian alirejea Marekani na kujipata tena anakuwa mwathiriwa kwa mara nyingine, wakati huu mwathiriwa wa gazeti la udaku lililochapisha msururu wa makala gazetini mapema Oktoba 2016 likimweleza kama mwongo na mwizi."

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kardashian aliibiwa akiwa Rue Tronchet, Paris

"Makala hizo zilidai, bila msingi wowote kwamba Kardashian aliigiza wzi huo na kwamba alidanganya kuhusu kushambuliwa na wezi hao na kisha akawasilisha dai kwenye kampuni ya bima ili kujipatia mamilioni ya dola."

Bw Mwangaguhunga alikataa kuomba radhi kwa kumuita "mwongo na mhalifu", nyaraka za mahakama zinasema.

MediaTakeout kufikia sasa hawajazungumzia kesi hiyo

Kardashian, 35, ameolewa na mwanamuziki Kanye West na wamejaliwa watoto watatu. Alipata umaarufu mkubwa kutokana na kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye televisheni cha Keeping up with the Kardashians.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii