Kwa Picha: Mafuriko Carolina Kaskazini kutokana na Kimbunga Matthew

Derrick Williams asaidiwa MLK Freeway baada ya kuokolewa kutoka kwenye maji ya mafuriko yaliyosababishwa na Kimbunga Matthew Oktoba 8, 2016 Fayetteville, N.C Haki miliki ya picha AP
Image caption Derrick Williams asaidiwa MLK Freeway baada ya kuokolewa kutoka kwenye maji ya mafuriko yaliyosababishwa na Kimbunga Matthew Oktoba 8, 2016 Fayetteville, N.C

Mafuriko makubwa yameshuhudiwa katika jimbo la Carolina Kaskazini, baada ya kimbunga Matthew kusababisha mvua kubwa katika jimbo hilo.

Kimbunga hicho kimesababisha vifo vya watu 35 kufikia sasa, 17 wakifariki katika jimbo hilo la Carolina Kaskazini.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kanisa lililofurika maji eneo la Lumberton, Carolina Kaskazini laonekana 11 Oktoba, 2016.
Haki miliki ya picha Reuters

Gavana Pat McCrory ameonya kuwa mafuriko hayo yataendelea kwa kipindi cha saa 72 zijazo katika baadhi ya maeneo ya jimbo hilo huku maji katika mito mingi yakiendelea kuongezeka.

Maafisa wa huduma za dharura wanasema watu 2,000 wameokolewa na wengine 4,000 wamepewa hifadhi ya muda.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanamume akitembea kwene maji ya mafuriko Lumberton, Carolina Kaskazini 10 Oktoba, 2016.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Afisa FEMA amsaidia mtoto na mbwa wake Lumberton, Carolina Kaskazini 10 Oktoba, 2016.

Baadhi ya sehemu za barabara ya Interstate 95, ambayo hupitia katika jimbo la Karolina Kaskazini bado zimefungwa.

Gavana huyo amewahimiza wakazi kutii amri ya kuondoka maeneo yaliyo hatarini na kutoendesha magari kwenye maeneo ambayo yamefurika maji.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Barabara ya Interstate 95 ikiwa imefunikwa na maji Lumberton, Carolina Kaskazini
Haki miliki ya picha AP
Image caption Jeremy Spearman atazama uharibifu uliosababishwa na mafuriko nyumbani mwake

"Watu wengi sana wamefariki. Na hatutaki wengine wafariki," aliambia wanahabari Jumanne.

Miongoni mwa waliotakwia kuhama Jumanne ni wakazi wa Cane Creek, kwa sababu bwawa linalozuia maji kwenye ziwa lililo karibu linakaribia kuvunja kingo zake, maafisa wa serikali ya jimbo la Moore waliambia News Observer.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Gari ya kutoa mafunzo ya udereva lakwama kwenye maji ya mafuriko
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mkazi atembea kwenye maji mafuriko Lumberton, Carolina Kaskazini

Mmoja wa watu waliopewa hifadhi, Wendy Key, ameambia Reuters kwamba alikimbia nyumba yao walioyokuwa wameipamba upya akiwa na watoto wake kutoroka mafuriko.

Kakake alimwambia kwamba maji kwenye nyumba yao sasa yanafika kiunoni.

Haki miliki ya picha Curtis Compton
Image caption Eneo la kihistoria la Ngome ya Pulaski limezingirwa na maji Savannah Georgia
Haki miliki ya picha AP
Image caption Watu watazama uharibifu uliotokea kwenye barabara ya Bingham eneo la Fayetteville, NC, Jumaili tarehe 9 Oktoba, 2016.

Zaidi ya nyumba na biashara 532,000 zilikwa hazina umeme kufikia Jumanne.

Rais Barack Obama ametangaza janga katika wilaya 31 za Carolina Kaskazini, kuwezesha pesa za serikali ya taifa kutumiwa kuwasaidia waathiriwa.