Mawakili wasema hawatamtetea mshukiwa wa Paris

Picha za Salah Abdeslam Haki miliki ya picha Belgian/French police
Image caption Abdeslam alikamatwa mwezi Machi karibu na mji wa Brussels

Mawakili wa mshukiwa mkuu wa shambulio la kigaidi lililotekelezwa mjini Paris Novemba mwaka jana, Salah Abdeslam, wamesema hawatamtetea tena.

Abdeslam anapanga kutumia haki yake ya kukaa kimya kortini, mmoja wa mawakili wake, Frank Berton, ameambia BFM TV.

"Tulisema tangu mwanzo ... kwamba mteja wetu akiamua kukaa kimya tutajiondoa," amesema, akiwa ameandamana na wakili mwenzake Sven Mary.

Watu 130 waliuawa wakati wa mashambulio hayo.

Kundi linalojiita Islamic State limedai kuhusika.

Salah Abdeslam alikamatwa mjini Brussels mwezi Machi na amesalia kimya tangu alipohamishiwa Ufaransa mwezi Aprili.

Image caption Mashambulio ya Paris