Wanaume Marekani kutengewa nafasi vyooni kuwabadili watoto ubinda

ishara ya eneo la kumabdilisha mtoto ubinda Haki miliki ya picha Thinkstock

Vyoo vya wanaume katika maeneo ya umma Marekani ni lazima sasa vitengewe nafasi ya kuwabadili watoto ubinda, kwa mujibu wa sheria mpya iliyotiwa saini na rais Barack Obama.

Vyoo vyote vya wanawake na wanaume vinapaswa "kuwa salama, safi, na vinavyofaa" kuwabadili watoto ubinda.

Sheria hiyo iliyopewa jina Vyoo vinavyopatikana katika hali zote (BABIES) iliwasilishwa mara ya kwanza mnamo Aprili na mbunge David N Cicilline.

"Mijengo ya serikali inafadhiliwa walipa kodi," anasema.

Haki miliki ya picha AFP/Getty Images

"Ni muhimu kuhakikisha kwamba sehemu hizo zipo wazi zinapatikana, na zenye kujali maslahi ya familia iwezekenavyo."

Sheria hii inafanya maenoe hayo ya umma "kujali maslahi ya baba na mama wanaofanya kazi" kote Marekani.

Hakuna sheria maalum Uingereza kuhusu meneo ya kuwabadili watoto ubinda, Raymond Martin, mkurugenzi wa British Toilet Association (BTA) anasema.

Shirika hilo liliundwa miaka 20 iliopita kupiganiavyoo bora vya umma nchini.

Wakati huo, anakadiria kuwa ni choo kimoja kati ya vyoo kumi vya wanaume vilikuwa vimetengewa nafasi ya kuwabadili watoto ubinda na kuwafanyia usafi. HIvi sasa ni zaidi ya thuluthi mbili.

Haki miliki ya picha Thinkstock

"Hili ni jambo lililopuuzwa," ameiambia BBC.

"Tumekuwa tukishirikiana na mashrika mengi na kampuni kubwa za utengenezaji bidhaa wanaotufuata kwa ushauri na muongozo."

Lakini anishutumu serikali, akieleza kuwa 'hazitaki kuwajibika' katika kuhakikisha Uingereza ina sehemu za kutosha.

Na mojawapo ya wasiwasi mkuu, Martin anasema, ni kiwango cha vyoo vya umma vinavyofungwa katika miaka ya hivi karibuni.