Wavuvi waombwa kuwasaka samaki 80,000 waliotoweka

Rainbow trouti Haki miliki ya picha AFP
Image caption Inahofiwa samaki hao wa trouti huenda wakayala mayai ya samaki wengine

Hadi samaki 80,000 aina ya rainbow trout wanaofugwa wameachiwa kimakosa baharini Denmark, na wito sasa umetolewa kwa wavuvi kujaribu kuwakamata.

Ajali hiyo imetokea wakati meli ya mizigo ilipogonga na kuingia katika sahmba la kufuga samaki katika eneo la Horsens Fjord katika rasi ya Jutland.

Kuna hofu kuwa samaki hao walio na uzito wa kilo 3, huedna wakatiza vizazi vya aina nyengine ya samaki.

Mwanamazingira mmoja ameomba "yoyote aliye na vifaa vya uvuvi... akavue".

Soren Knabe, mwenyekiti wa kundi la kimazingira Vandpleje Fyn na mwenyekiti wa muungano wa wavuvi Denmark, ameliambia gazeti la Copenhagen post kuwa huu ni muda mbaya zaidi kwa samaki hao kuingia katika bahari hiyo.

'Bahati mbaya'

Meli hiyo ya mizigo ilikuwa inatoka Kalinigard Urusi kuelekea katika bandari ya Kolding Denmark ilipoingia katika sahmba hilo la ufugaji samaki.

Jon Svendsen, mtafiti wa taasisi ya National Institute of Aquatic Resources, amesema samaki hao ni tisho kwa kizazi cha samaki wa baharini kwasababu wanaweza kuchimba kutafuta mayai ya samaki na kuyala.

Amesema hiyo inaweza kuathiri moja kwa moja mazingira nani 'bahati mbaya' ajali hii imetokea sasa.

Dr Svendsen ameshinikiza wito kuwa wavuvi wajaribu kuwavua samaki hao. Hatahivyo amesema tihiso hilo sio la muda mrefu.

Tishio kubwa zaidi kwa mazingira amesema ni kuchotwa mchanga wa baharini kwa ujenzi , shughuli za viumbe visivyo vya baharini, mabadiliko ya hali ya hewa na mashamba yenyewe ya kufuga samaki.

"Mashamba ya samaki ni hatari zaidi kwa mazingira ya baharini,hususan kwasababu ya virutubishaji vinavyosambaa, ambavyo vinahusika kupungua kwa hewa safi ya oxygen hali inayofahamika kama subsequent hypoxia," Dr Svendsen ameiambia BBC.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii