Simba na Yanga zashinda Azam yachapwa

Simba Haki miliki ya picha Google
Image caption Wachezaji wa wekundu wa Msimbazi Simba

Wekundu wa msimbazi Simba Wakicheza ugenini katika dimba la Sokoine waliibuka na ushindi mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City.

Timu ya wanainchi Dar young Africans nao wakachomoza na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wakatamiwa na Mtibwa Sugar.

Mwadui Fc wakawachapa African Lyon kwa mabao 2-0. Chama la wana Stand United wamewachapa wanalamba lamba Azam FC kwa bao 1-0.

Jkt Ruvu na Tanzania Prisons wametosha nguvu kwa sare ya bila kufungana. Nao Mbao Fc waliwachapa ndugu zao Toto Africans kwa mabao 3-1

Majimaji wamelala nyumbani kwa kuchapa kwa bao 1-0 na kagera Sugar.Ligi hiyo itaendelea tena leo hii kwa mchezo mmoja kupigwa Kwa Ruvu Shooting kuwa wenyeji wa Ndanda.