Kwa picha: Maisha ya Mfalme Bhumibol Adulyadej

Mfalme Bhumibol Adulyadej wa Thailand ndio kiongozi aliyehudumu kwa muda mrefu katika kiti cha ufalme anayeonekana kuwa na ushawishi ulio imarika katika nchi ambayo imeshuhudia mapinduzi kadhaa, katiba 17 na mawaziri wakuu wengi.

Haki miliki ya picha AP

Mfalme Bhumibol Adulyadej (kushoto) alipokea madaraka Juni 9 1946 baada ya kakake, Mflame Ananda Mahidol (kulia), kufariki katika ajali iliotokea wakati wa ufyetuaji risasi katika kasri kuu Bangkok. Wanaonekana katika picha hii mnamo 1935 wakiwa shuleni Lausanne, Uswizi.

Haki miliki ya picha AP

Mfalme Bhumibol Adulyadej alizaliwa Cambridge, Massachusetts, ambako babake alikuwa anasoma, na baadaye alisomea Uswizi. Alikutana na mkewe Mwanamfalme Sirikit, akiwa Ulaya.

Haki miliki ya picha AP

Wanandoa hao walizaa watoto 4, lakini wanaonekana hapa 1955 na Mwanamfalme Vajiralongkorn na Ubol Ratana. Hadhi ya ufalme huo ilishuka tangu kuondolewa kwa utawala wa kifalme 1932 na baada ya kuachia madaraka Mfalme Prajadhipok, mjombake Mfalme Bhumibol mnamo 1935.

Haki miliki ya picha AP

Mfalme Bhumibol alijenga upya hadhi ya Ufalme kupitia ziara kadhaa katika majimbo, kupitia miradi tofuati yaliodhihirisha wasiwasi wake wa muda mrefu kuhusu maendeleo ya kilimo. Alionekana pia na viongozi wa dunia, hapa na rais wa Marekani Dwight Eisenhower alipokuwa katika ziara Washington.

Haki miliki ya picha PA

Na hapa na Malkia Elizabeth London 1960.

Haki miliki ya picha AP

1972 Malkia naye aliizuru Thailand kwa siku tano.

Haki miliki ya picha AP

Mfalme Bhumibol aliingilia kati kwa mara ya kwanza mzozo wa kisiasa Thailand mnamo 1973, wakati waandamanaji wanaounga demokrasia mkono walipo shambuliwa kwa risasi na wanajeshi, na waliruhusiwa kujificha kwenye kasri, hatua iliosababisha kuanguka utawala wa aliyekuwa waziri mkuu Jenerali Thanom Kittikachorn.

Haki miliki ya picha AP

1981, Mfalme Bhumibol aliingilia kati mzozo wa kisiasa na kupinga wanajeshi waliompindua waziri mkuu na ambaye ni rafiki wa karibu wa Mfalme, Jenerali Prem Tinsulanond (kushoto). Vikosi vinavyoutii ufalme vilidhibiti upya Bangkok.

Haki miliki ya picha AP

Mfalme Bhumibol alifurahia mambo tofauti ikiwemo upigaji picha, kucheza na kutunga nyimbo, kupuliza saxafoni, kuchora na kuandika. Hapa anapuliza saxafoni na mwanawe Mwana mfalme Vajiralongkorn, na wanamuziki wengine. Anafurahia kucheza jazz na wasanii wengine kama Benny Goodman, Stan Getz, Lionel Hampton na Benny Carter.

Haki miliki ya picha AP

Wakati wa mzozo uliozuka dhidi ya aliyekuwa waziri mkuu Thaksin Shinawatra mnamo 2006, Mfalme aliombwa mara kadhaa kuingilia kati hali, lakini alisistiza kuwa haitokuwa sawa.

Haki miliki ya picha AP

Mwaka mmoja baadaye Desemba 5 2007, taifa liliadhimisha miaka 80 ya mfalme Bhumibol.

Haki miliki ya picha AP