Wasichana wa Chibok walibadilishwa na makamanda

Wasichana wa Chibok walioachiliwa walibadilishwa na makamanda wa Boko Harama waliokuwa wamekamatwa na serikali kulingana na mtandao wa Sahara
Image caption Wasichana wa Chibok walioachiliwa walibadilishwa na makamanda wa Boko Harama waliokuwa wamekamatwa na serikali kulingana na mtandao wa Sahara

Mtandao wa habari wa Sahara ambao ulikuwa wa kwanza kuripoti kuhusu kuachiliwa kwa wasichana wa Chibok umechapisha ujumbe katika mtandao wake wa Twitter kuhusu ubadilishanaji wa wafungwa uliosababisha kuachiliwa kwao.

Maelezo bado hayajathibitishwa ,lakini mtandao huo unasema kuwa wasichana 18 wana watoto na kwamba walibadilishwa na makamanda wanne wa Boko haram .

Pia mtandao huo umeripoti kwamba wasichana hao wanaelekea mji mkuu wa Abuja.