Uagizaji wa kuku watishia wafugaji Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Uagizaji wa kuku kutoka nje watishia wafugaji Tanzania

Katika mwendelezo wa makala ya ufugaji kuku, leo ni nchini Tanzania ambapo kwa miaka ya hivi karibuni watu kutoka katika makundi tofauti ya kijamii wamejiingiza katika ufugaji wa kuku, kama moja ya harakati za kujikwamua kiuchumi.

Hata hivyo, uagizaji wa kuku kutoka nje ya nchi, wanasema kuwa ni hatua ya kuwarudisha nyuma kiuchumi wafugaji wa ndani.

Mwandishi wetu Aboubakar Famau ametuandalia taarifa ifuatayo.