Mshike mshike wa ligi ya England kuendelea kesho

Ligi kuu ya England inaendelea tena wikiendi hii kwa michezo saba kucheza baada kusimama kupisha michezo ya kimataifa.

Haki miliki ya picha Google
Image caption Wachezaji wa Leicester City

Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Leicester City, watakua ugenini Stanford Bridge, kuwakabali wenyeji Chelsea.Washika bunduki wa London Arsenal wao watakua nyumbani katika dimba la Emirate kuwalika Swansea City.

Matajiri wa jiji la Manchester Man City, watawakaribisha Everton mchezo utakaopigwa katika dimba la Etihad, Fc Bournemouth wao watakipiga na Hull city.

Stoke City watakua nyumbani katika dimba la Britania kucheza na Paka Weusi wa Sunderland, West Bromwich Albion watapima ubavu na Tottenham.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wachezaji wa wagonga nyundo wa London West Ham United

Wagonga nyundo wa London West Ham United watakua na kibarua pevu kwa kupepetana na Tai wa Crystal Palace.