Muda wa kusitishwa mapigano waongezwa Colombia

Juan Manuel Santos
Image caption Rais wa Colombia Juan Manuel Santos

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos ametangaza kuwa anaongeza muda wa kusitisha mapigano na kundi la waasi la FARC hadi mwisho wa mwaka huu.

Anataka kutoa muda zaidi wa jitihada za kuokoa makubaliano yaliyosainiwa pamoja na kundi la FARC mwezi uliopita.

Makubaliano hayo yaliingia doa baada ya kura ya maoni huku baadhi ya wananchi walipiga kura ya hapana.

Rais Santos siku chache zilizopita amekua akifanya mkutano na waliojihusiha na kampeni ya kupiga kura ya hapana iliyoongozwa na Rais aliyeondoka madarakani Alvaro Uribe, wanataka kupitia upya mkataba huo wa amani ambao umechukua zaidi ya miaka minne ya makubaliano.

Santos amesema kuwa ana matumaini ya kufikia makubaliano kabla ya kuisha kwa tarehe ya kuisha kwa usitishwaji wa mapigano.