Samsung kupoteza faida ya £4.4bn kutokana na Note 7

Samsung Note 7 Haki miliki ya picha AFP

Kampuni ya Samsung imesema gharama ya kuacha kuuza simu yake ya karibuni zaidi ya Galaxy Note 7 sitakuwa zaidi ya £4.4bn ($5.4bn).

Kampuni hiyo ya Korea Kusini tayari imepunguza matarajio yake ya faida ya robo ya tatu ya mwaka kwa £1.9bn ($2.3bn).

Mnamo Ijumaa, kampuni hiyo ilisema inatarajia kuathirika zaidi na kupoteza won 3.5 trilioni zaidi ($3bn, £2.5bn).

Samsung iliwashauri wateja waliokuwa wamenunua Note 7 warejeshe simu walizokuwa wamenunua baada ya visa vya simu hizo kulipuka na kuwaka moto kuripotiwa.

Hitilafu ilidhaniwa kuwa kwenye betri.

Kampuni hiyo hata hivyo iliacha kuunda na kutengeneza simu hizo baada ya simu mpya walizokuwa wamebadilishiwa wateja, ambazo zilidhaniwa kuwa salama, kuanza kushika moto.

Simu hiyo ilikuwa imezinduliwa Agosti ikitarajiwa kushindana na simu mpya ya Apple iPhone7.

Licha ya matatizo hayo, Samsung Electronics imesema inatarajia kupata faida ya won 5.2 trilioni (£3.7bn) robo ya tatu ya mwaka huu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Simu ya Samsung Note 7 ilishika moto ikifanyiwa uchunguzi kwenye maabara Singapore

Simu hiyo imesema itajaribu kuuza zaidi simu zake nyingine kama vile Galaxy S7 na S7 Edge ili kukwamua biashara.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii