Je Aisha Buhari ni nani?

Bi Aisha Buhari akipiga kura wakati wa uchaguzi mkuu nchini humo
Image caption Bi Aisha Buhari akipiga kura wakati wa uchaguzi mkuu nchini humo

Alizaliwa mnamo tarehe 17 mwezi wa Februari 1971 Kaskazini mashariki mwa Nigeria katika jimbo la Adamawa.

Aisha Buhari ni mjukuu wa waziri wa kwanza wa ulinzi nchini Nigeria Alhaji Muhammadu Ribadu.

Aliolewa na Muhammadu Buhari mwaka 1989.Wana watoto watano ,mvulana mmoja na wasichana wanne.

Mwaka 1995,alifungua jumba la Hanzy Spa,kaskazi mwa Nigeria ikiwa ndio jumba la kwanza la urembo ,huko Kaduna baada ya kufanikiwa kupata cheti cha Diploma ya urembo kutoka chuo kikuu cha Carlton nchini Uingereza.

Alichapisha kitabu ''Essential of Beauty Therapy'': Kielelezo kamili cha utaalam wa urembo 2014.

Ni wakili wa maswala ya haki za kibinaadamu na amefadhili fedha kuzisaidia familia za waathiriwa wa Boko Haram baada ya zaidi ya wasichana 250 kutekwa na wapiganaji hao 2014.

Aliwashangaza wengi mwaka uliopita baada ya kuonekana hadharani akiwa amevaa saa ya bei ghali,na kuwafanya baadhi ya raia kujiuliza iwapo alikuwa anakandamiza mpango wa rais Buhari kuonekana mtu wa watu.

Bi Buhari pia alikosolewa katika mitandao ya kijamiii kwa kujaribu kusalimiana kwa mkono na Alaafin of Oyo,Chifu wa watu wa Yoruba.