Wanajeshi 12 wauawa na wapiganaji Misri

Eneo la shambulio hilo lililodaiwa kutekelezwa na wapiganaji
Image caption Eneo la shambulio hilo lililodaiwa kutekelezwa na wapiganaji

Maafisa wa usalama nchini Misri wanasema kuwa watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kiislamu wamewaua wanajeshi 12 wakati wa shambulizi katika kuzuizi cha jeshi eneo la rasi ya Sinai.

Wanajeshi 8 walijeruhiwa wakati wa shambulizi hilo lililotokea karibu na mji wa Beir al-Abd.

Kulingana na jeshi nao washambuliaji 15 waliuawa

Wanamgambo hao wanaongozwa wa tawi la eneo hilo la kundi la Islamic State.