Kwa Picha: Afrika wiki hii 7 - 13 Oktoba 2016

Huu hapa ni mkusanyiko wa picha bora za matukio Afrika wiki hii:

Mfuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini Ghana New Patriotic Party wakati wa uzinduzi wa manifesto ya chama hicho Jumapili mjini Accra. Uchaguzi mkuu nchini humo utafanyika Desemba. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mfuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini Ghana New Patriotic Party (NPP) wakati wa uzinduzi wa manifesto ya chama hicho Jumapili mjini Accra. Uchaguzi mkuu nchini humo utafanyika Desemba.
Mali waliungwa mkono vyema na mashabiki wao ugenini mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast uwanja wa Stade de la Paix mjni Bouake Jumamosi. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mali waliungwa mkono vyema na mashabiki wao ugenini mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast uwanja wa Stade de la Paix mjni Bouake Jumamosi.
Lakini mambo hayakuwaendea vyema mashabiki hao wageni kwani Ivory Coast walilaza Mali 3-1. Huyu hapa ni shabiki wa Ivory Coast. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Lakini mambo hayakuwaendea vyema mashabiki hao wageni kwani Ivory Coast walilaza Mali 3-1. Huyu hapa ni shabiki wa Ivory Coast.
Mjini Addis Ababa, hawa ni waumini wa kanisa la Kilutheri wakiinua mikono Jumapili wakati wa ibada ya kuwakumbuka waliofariki wakati wa tamasha ya kidini ya jamii ya Oromo wiki iliyotangulia. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mjini Addis Ababa, hawa ni waumini wa kanisa la Kilutheri wakiinua mikono Jumapili wakati wa ibada ya kuwakumbuka waliofariki wakati wa tamasha ya kidini ya jamii ya Oromo wiki iliyotangulia.
Nchini Liberia mnamo Jumanne, wafuasi wa mhubiri kutoka Nigeria Johnson Suleman wakiwa kwenye ibada uwanja mkuu wa michezo Monrovia. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Nchini Liberia mnamo Jumanne, wafuasi wa mhubiri kutoka Nigeria Johnson Suleman wakiwa kwenye ibada uwanja mkuu wa michezo Monrovia.
Watu walikuwa na hamu sana ya kuingia, na wengine walipitia juu ya ua, kumsikiliza mhubiri huyo kutoka Nigeria. Ibada hiyo iliandaliwa na kanisa la Omega Fire Ministries . Haki miliki ya picha EPA
Image caption Watu walikuwa na hamu sana ya kuingia, na wengine walipitia juu ya ua, kumsikiliza mhubiri huyo kutoka Nigeria. Ibada hiyo iliandaliwa na kanisa la Omega Fire Ministries .
Jumatano, mwanafunzi wa Afrika Kusini aliyekuwa akiandamana azungumza na polisi wa Fanya Fujo Uone nje ya mahakama Johannesburg ambapo wanafunzi kadha waliokamatwa wakati wa maandamano ya awali walikuwa wanafikishwa kortini. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jumatano, mwanafunzi wa Afrika Kusini aliyekuwa akiandamana azungumza na polisi wa Fanya Fujo Uone nje ya mahakama Johannesburg ambapo wanafunzi kadha waliokamatwa wakati wa maandamano ya awali walikuwa wanafikishwa kortini.
Katika kituo cha kupigia kura viungani mwa mji wa Rabat, Morocco, watu wanasubiri kupiga kura kwenye uchaguzi wa ubunge Ijumaa tarehe 7 Oktoba. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Katika kituo cha kupigia kura viungani mwa mji wa Rabat, Morocco, watu wanasubiri kupiga kura kwenye uchaguzi wa ubunge Ijumaa tarehe 7 Oktoba.
Siku iyo hiyo, mjini Accra, Ghana, mwanamitindo anapodolewa kabla ya kushiriki maonyesho ya mitindo ya Accra Fashion Week mnamo Oktoba 7, 2016. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Siku iyo hiyo, mjini Accra, Ghana, mwanamitindo anapodolewa kabla ya kushiriki maonyesho ya mitindo ya Accra Fashion Week mnamo Oktoba 7, 2016.
Eneo la Aweil, Sudan Kusini, wachuuzi wanauza vyakula sokoni Alhamisi. Uhaba wa bidhaa sokoni ni ishara ya mavuno duni yaliyoshuhudiwa msimu wa kuvuna uliopita. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Eneo la Aweil, Sudan Kusini, wachuuzi wanauza vyakula sokoni Alhamisi. Uhaba wa bidhaa sokoni ni ishara ya mavuno duni yaliyoshuhudiwa msimu wa kuvuna uliopita.
Jumamosi, fundi wa vyuma mjini Monrovia, Liberia alikuwa anamalizia kuunda toroli ambayo anatarajia atauza karibuni. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Jumamosi, fundi wa vyuma mjini Monrovia, Liberia alikuwa anamalizia kuunda toroli ambayo anatarajia atauza karibuni.
Na katika mji wa Sirte, Libya, wapiganaji wanaohusishwa na serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa waliteka jengo ambalo awali lilidhibitiwa na wapiganaji wa Islamic State mnamo Jumatatu. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Na katika mji wa Sirte, Libya, wapiganaji wanaohusishwa na serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa waliteka jengo ambalo awali lilidhibitiwa na wapiganaji wa Islamic State mnamo Jumatatu.
Libya pia imekuwa ikitumiwa na maelfu ya wahamiaji wanaotaka kufika Ulaya. Jumatano, mwanamke huyu, na abiria wengine, waliokolewa kutoka kwa boti lililokuwa linazama bahari ya Mediterranean. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Libya pia imekuwa ikitumiwa na maelfu ya wahamiaji wanaotaka kufika Ulaya. Jumatano, mwanamke huyu, na abiria wengine, waliokolewa kutoka kwa boti lililokuwa linazama bahari ya Mediterranean.

Images courtesy of AP, AFP, EPA, PA and Reuters