Raia wa Thailand waomboleza kifo cha mfalme Bhumibol

Raia wa Thailand waomboleza kifo cha mfalme Bhumibol
Image caption Raia wa Thailand waomboleza kifo cha mfalme Bhumibol

Maelfu ya waombolezaji wa Thai wanapanga foleni katika barabara za miji ya Bangkok ,wakiwa na matumaini ya kuuona mwili wa wa mfalme Bhumibol Adulyadej wakati ulipkuwa ukitolewa hospitalini na kuelekea katika hekalu katika nyumba yake.

Image caption Jeshi la serikali ya Thailand likifanya gwaride la kutoa heshima kwa mfalme huyo

Mfalme huyo aliyetawala kwa muda mrefu zaidi duniani alifariki siku ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 88,na kusababaisha majonzi makubwa ya kitaifa.

Serikali imetangaza mwaka mzima wa kuomboleza.

Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Waombolezaji katika maeneo tofauti ya Thailand wakimuenzi marehemu Bhumibol

Mwanamfalme Mah Wajiralongkorn ndio atakayemrithi ,lakini ametaka kucheleweshwa kwa mpango huo.

Image caption Familia ya Ufalme nchini Thailand

Baraza la mawaziri limeangza Ijumaa kuwa siku kuu,na bendera zinapepea katika nusu mlingoti kwa siku 30.

Image caption Watu wametakiwa kuva nguo nyeusi wakati huu wa maombolezi

Watu wametakiwa kuvaa nguo nyeusi na kutoshiriki katika matukio ya furaha wakati huu.

Kumbi za sinema,tamasha na michezo imefutiliwa mbali au hata kuahirishwa.

Image caption Mwanamfalme atakayemrithi Mfalme Bhumibol