Watu 30 wauawa mkusanyiko wa Washia Iraq

Shambulio Baghdad Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua akiwa ndani ya hema

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga ameshambulia mkusanyiko wa Waislamu wa madhehebu ya shia kwenye hema mji mkuu wa Iraq, Baghdad.

Watu zaidi ya 30 wameuawa na wengine sitini kujeruhiwa.

Hema hilo lilikuwa kwenye soko lenye watu wengi kaskazini mwa mji wa Baghdad.

Washia wengi wanaendelea na matambiko ya kuomboleza kama sehemu ya kuadhimisha kuuawa kwa mjukuu wa Nabii Mohammed, Hussein, karne ya saba.

Wapiganaji wa kundi linalojiita Islamic State wamedai kuhusika.

Wamekuwa wakitekeleza mashambulio ya aina hiyo miezi ya karibuni Baghdad huku kundi hilo likiendelea kupoteza udhibiti wa maeneo Iraq.