Uganda mbele kwa ujasiriamali Afrika
Huwezi kusikiliza tena

Uganda mbele kwa ujasiriamali Afrika

Ukitazama, Marekani inaonekana kuwa ndio kinara wa ubepari duniani, na pengine kiongozi wa ubunifu na ujasiriamali.

Lakini utafiti wa karibuni unaonyesha kati ya watu wazima wanaojiingiza katika ujasiriamali barani Afrika, Uganda ndiyo inayoongoza.

Lakini biashara chache tu zilizoanzishwa nchini humo zimefanikiwa kudumu.

Mwandishi wetu Nancy Kacungira alikwenda Uganda ambako vijana wamebuni fursa mbalimbali za ujasiriamali na kuifanya Uganda kuwa kitovu cha umiliki wa biashara zilizobuniwa ndani ya nchi.