Ndege zisizo na rubani kusafirisha damu Rwanda
Huwezi kusikiliza tena

Ndege zisizo na rubani kusafirisha damu Rwanda

Kwa mara ya kwanza duniani, damu itaweza kusafirishwa hadi maeneo ya mbali nchini Rwanda, kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani.

Kampuni moja ya Marekani, Zipline, itazitumia ndege hizo zinazotumia mawasiliano ya satelaiti, kuvuka milima na kutumia muda mfupi sana ikilinganishwa na usafiri wa barabara.

Pakiti hizo zenye damu zitarushwa chini kwa kutumia parachuti ambazo hatimaye huweza kuoza kwa haraka. Idara ya afya ya Rwanda italipa gharama za kila mzigo unaoangushwa kwa ndege.

Ikiwa mpango huu utafanikiwa, ndege hizi pia zitaanza kusafirisha chanjo na mahitaji mengine ya matibabu yanayohitajika kwa haraka.

Mwandishi wa BBC Yves Bucyana ana maelezo zaidi.