Watu 10 zaidi wafariki CAR

Duru za habari kutoka Jamhuri ya Afrika ya kati, zinasema kuwa yamkini watu 10 wameuwawa katika shambulio dhidi ya kambi moja ya wakimbizi iliiyoko katikati mwa kijiji cha Ngakobo.

Image caption Wapiganaji wa Seleka

Haijafahamika mara moja ni nani aliyetekeleza shambulio hilo, lililofanyika majira ya usiku.

Linatukia siku tatu tu, baada ya karibu watu thelathini kuuwawa katika shambulio kwenye kambi nyingine ya wakimbizi wa ndani kwa ndani nchini humo.

Makao makuu ya Umoja wa mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya kati, inalilaumu kundi kuu la wanamgambo wa kiislamu wa Seleka, kwa shambulio la Jumatano iliyopita.

Taifa hilo lingali linajinasua kutoka katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, vilivyoanza mwaka 2013 na kuwafurusha makwao, robo ya raia wa nchi hiyo ya Afrika ya kati.