Waasi 'waiteka' ngome muhimu ya IS Syria

Waasi wanaoungwa mkono na serikali ya Uturuki waiteka ngome muhimu ya IS ya Dabiq
Image caption Waasi wanaoungwa mkono na serikali ya Uturuki waiteka ngome muhimu ya IS ya Dabiq

Waasi wanaoungwa mkono na serikali ya Uturuki nchini Syria wameuteka mji muhimu wa Dabiq kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State,kulingana na makamanda wa waasi hao na wachunguzi.

Waasi hao waliuteka mji wa Dabiq baada ya wanachama wa kundi la Islamic State kuuondoka kulingana na kundi la haki za kibinaadamu lililo na makao yake huko Uingereza.

Mji huo mdogo wa Kaskazini una thamani kubwa kwa IS kwa sababu umekuwa ukitajwa katika ubashiri mwingi wa vita vya kundi hilo pamoja na propaganda zake.

Utekaji wa mji huo ni miongoni mwa vita vikali vilivyoanzishwa na makundi ya waasi nchini Syria dhidi ya kundi hilo.