Mafuriko yauwa watu 21 Vietnam

Mafuriko Vietnam Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mafuriko Vietnam

Mafuriko makubwa katikati mwa taifa la Vietnam yamesababisha vifo vya watu 21 huku makumi ya maelfu ya nyumba yakizama.

Mkoa wa Quang Binh ndio ulioathirika sana huku watu 11 wakifariki ,mimea kuharibiwa na mifugo ikisombwa na maji.

Mafuriko hayo yamesababishwa na mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha ,lakini vyombo vya habari vinasema kuwa maji yaliotoka katika hifadhi za umeme yalichangia pakubwa mafuriko hayo.

Kimbunga Sarika huenda kikasababisha hali mbaya ya anga iwapo kitapiga Vietnam.

Siku ya Jumapili kimbunga hicho kilipita katika kisiwa cha Luzon na kuelekea katika bahari ya kusini mwa China.

Maelfu ya raia wa Filipino waliondoka katika maeneo ya chini huku kuharibika kwa mali,kuzama kwa miti ya stima na kuanguka kwa miti kukiripotiwa.