Mwana wa Tyson Gay afariki baada ya kupigwa risasi

Mwanariadha wa mbio za mitaa 100 wa Marekani Tyson Gay
Image caption Mwanariadha wa mbio za mitaa 100 wa Marekani Tyson Gay

Mwana wa mwanariadha wa mbio fupi nchini Marekani Tyson Gay ameuawa katika ufyatulianaji wa risasi katika jimbo la Kentucky kulingana na polisi na vyombo vya habari.

Maafisa wa polisi huko Lexington wamesema kuwa Trinity Gay alipigwa risasi shingoni wakati wa ufyatulianaji huo wa risasi kati ya magari mawili yaliokuwa katika eneo moja la kuegesha magari la mkahawa mmoja.

Alikimbizwa hospitalini ambapo alifariki .

Bwana Gay ambaye anatoka eneo la Lexington alithibitisha kifo chake kwa runinga ya Lex 18.