Syria: IS wasambaratishwa katika mji wa Dabiq

Mji wa Dabiq unashikiliwa na waasi
Image caption Mji wa Dabiq unashikiliwa na waasi

Wapiganaji wa Free Syria Army, wakisaidiwa na mizinga na ndege za kivita za Uturuki, wamewafurusha Islamic State kutoka mji muhimu wa Dabiq karibu na mpaka wa Uturuki.

Walikumbana na upinzani kidogo. Msemaji wa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kurudisha mji huo ulikuwa ni mkakati na ni ushindi muhimu.

Aidha amesema Uturuki itaendelea na Operesheni yake nchini Syria mpaka itakapothibitisha mipaka yake ipo salama.

Wakati huohuo, mapigano yameendelea katika mji wa Alepo.

Ripoti zinasema kwamba kumekuwa na mashambulizi ya anga yasiyosita katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi mjini Alepo.