Hatimaye Wasichana wa Chibok waungana na familia zao

Wasichana wa Chibok, Nigeria Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wasichana wa Chibok, Nigeria

Wasichana wa shule 21 ambao walitekwa na wapiganaji wa kiislamu katika mji wa Chibok hatimaye wameungana tena na familia zao.

Wasichana hao waliokuwa wakishikiliwa kwa takriban miaka miwili na wapiganaji wa Boko Haram wamesimulia mateso waliyopitia.

Mmoja wa wasichana hao anasema alidhani kuwa siku ya kuachiwa kwake haitakuja kutokea. Huku mzazi mmoja wapo akisema kwamba wanaendelea kuwaombea dua wasichana ambao bado wanashikiliwa.

Msemji wa Rais wa Nigeria Garba Shehu ameliambia Shirika la Habari la Reuters wapiganaji ambao waliwaachia wasichana hao siku ya Alhamisi bado wanawashikilia wasichana wengine wapatao 83.

Zaidi ya wanafunzi 250 kutoka Chobok walikamatwa mateka April 2014.