Mwafalme wa mwisho wa Rwanda afariki dunia
Huwezi kusikiliza tena

Mfalme wa mwisho wa Rwanda, Kigeli V, afariki dunia

Mfalme wa zamani wa Rwanda Kigeli wa tano Ndahindurwa amefariki dunia akiwa uhamishoni nchini Marekani.

Mfalme huyo alitawala Rwanda kwa miaka miwili tu kwanzia mwaka 1959 hadi 1961 wakati utawala wa kifalme ulipong'olewa kupitia kura ya maamuzi na kumlazimisha kwenda uhamishoni.

Hata hivyo hakuweza kurejea nchini mwake kwa kutofautiana na utawala uliopo sasa nchini Rwanda.

Kutoka Kigali mwandishi wa BBC Yves Bucyana ametuma taarifa ifuatayo.