Kenya Airways yafuta safari za ndege
Huwezi kusikiliza tena

Kenya Airways yafuta safari za ndege

Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways, limefuta safari kadha za ndege zake hadi nchi mbalimbali za Afrika.

Shirika hilo, ambalo linakabiliwa na matatizo ya kifedha, lilichukua hatua hiyo kutokana na ukosefu wa wafanyakazi wa kutosha.

Kenya Airways inakabiliwa na uwezekano wa kutatizika zaidi kutokana na mgomo wa marubani ambao wametishia kugoma kuanzia Jumanne kushinikiza kujiuzulu kwa wakuu wa shirika hilo.

Mwandishi wa BBC Muliro Telewa anaarifu zaidi.