Wazee wanavyoishi maisha ya dhiki Mtwara, Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Wazee wanavyoishi maisha ya dhiki Mtwara, Tanzania

Umaskini katika nchi nyingi za Afrika, huwafanya vijana wengi hususan wa vijijini kukimbilia mijini au hata katika nchi zilizoendelea kwa lengo la kutafuta maisha bora.

Hali hii hufanya wazee wengi kuachwa bila matunzo yoyote na kuishia kujilea na wakati mwingine pia kuachiwa mzigo wa kulea wajukuu.

Halima Nyanza aliwatembelea baadhi ya wazee mkoani Mtwara kusini mwa Tanzania, kujionea maisha yao.