Afisi ya Republican yarushiwa bomu Marekani

Afisi ya chama cha Republican iliopigwa bomu katika kaunti ya Orange nchini Marekani
Image caption Afisi ya chama cha Republican iliopigwa bomu katika kaunti ya Orange nchini Marekani

Afisi moja ya chama cha Republican katika jimbo la North Carolina imeharibiwa na moto huku jengo lililo karibu yake likipakwa rangi ya nembo inayopinga chama cha Republican,mamlaka imesema.

Chupa iliojazwa mafuta yanayoweza kushika moto ilirushwa katika dirisha la makao makuu ya chama cha Republican kaunti ya Orange,chama hicho kimesema.

Mkurugenzi wa chama cha Republican, Dallas Woodhouse alisema kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa,na kwamba tahadhari ya kiusalama imetumwa katika afisi nyengine za chama hicho.

''Wanachama wa Nazi walio katika chama cha Republican ni sharti waondoke mjini''.

Mgombea wa Democrat Hillary Clinton ameandika katika mtandao wake wa Twitter kwamba shambulio hilo ni ''la kutisha na halitakubalika''.

Image caption Afisi ya chama cha Republican ilishambuliwa kwa bomu nchini Marekani

Lakini Mgombea wa chama cha Republican Donald Trump alionekana akiwalaumu wafuasi wa chama cha Democrat kwa kutekeleza kitendo hicho.

''Wanyama wanaomwakilisha Hillary Clinton huko North Carolina walirusha bomu katika ofisi yetu ya kaunti ya Ornge kwa sababu tunashinda'',alisema katika mtandao wake wa Twitter.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii