Liverpool kuchuana na Man United

Liverpool yaikaribisha nyumbani Manchester United
Image caption Liverpool yaikaribisha nyumbani Manchester United

Tatizo la nyonga huenda likamuweka nje Adam Lallana pamoja na Georginio Wijnaldum kwa upande wa Liverpool baada ya kujeruhiwa akichezea Uholanzi.

Mabeki Nathaniel Clyne na Dejan Lovren wamerudi huku Emre Can akitarajiwa kuanza kucheza kwa mara ya kwanza msimu huu.

Kiungo wa kati wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan na beki Luke Shaw wako tayari kuelekea Anfiled kufuatia majeraha.

Phil Jones ndio mchezaji wa pekee ambaye anauguza jereha katika kikosi ambacho hakina majeraha mengi.

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema: Mbali na jedwali la ligi ni mechi muhimu sana.Najua kuhusu historia ,napenda mechi maalum kama hizi. Kila mtu duniani ataitazama mechi hii.Ni heshima kubwa kuhusika.