Maisha na kifo cha ng'ombe wa kipekee Singapore

Lala mahali pema peponi Ngombe wa Kisiwa cha Coney
Image caption Lala mahali pema peponi Ngombe wa Kisiwa cha Coney

Ng'ombe wa kipekee na anayependwa na wengi nchini Singapore alifariki wiki iliopita.

Ngombe huyo aliyekuwa katika kisiwa cha Coney aliishi kwa miaka mingi, lakini kama anavyoelezea Heather Chen,ujio wake haujulikani na kifo chake kimezua huzuni.

Hakuna anayejua vile ng'ombe huyo alivyopata mauti yake katika kisiwa cha Coney.

Image caption Kisiwa cha Coney nchini Singapore

Mnyama huyo huenda alitangatanga .Lakini kwa kuwa hakuna mtu aliyeripoti ng'ombe wake aliyepotea,uwepo wake katika kiswa hicho ulikuwa wa kushangaza.

Kisiwa hicho chenye hekta 133 kilikuwa kikimilikiwa na ndugu Haw Par,wafanyibiashara matajiri ambao wameweka historia kubwa nchini Singapore.

Walikiuza kisiwa hicho 1950 kwa mfanyibiashara wa Kihindi ambaye alitaka kukiimarisha ili kufanana na New York.

Image caption Kisiwa cha Coney kina mandhari ya kujifurahisha

Lakini hakuna lililoonekana licha ya kubadilishwa jina,na ardhi hiyo ikapangiwa kufanyiwa maendeleo ya serikali.

Mwaka mmoja uliopita,kisiwa hicho kilikuwa mbuga mpya ya wanyama pori ,kikiruhusu matembezi ya muda mrefu pamoja na kupelekea baiskeli.

Ni wakati huo ambapo kila mtu aligundua kwamba kisiwa hicho kilikuwa cha mnyama mmoja maarufu: Ng'ombe.

Image caption Masharti yaliowekwa kwa watu wanaotaka kumuona Ngombe huo wa kipekee kisiwani Coney

Uwepo na ukakamavu wake ulimfanya ng'ombe huyo kuwa maarufu miongoni mwa raia wa Singapore ,wengi wao wakiishi katika makaazi ya mji na wasio na uzoefu wowote na mifugo.

Hakuna safari katika kisiwa cha Coney iliokamilika bila ya usakaji wa ng'ombe huyo huku raia wakitii sheria zilizowekwa za: kutomlisha,kutomchokoza na kutompiga picha.

Lakini kwa bahati mbaya maisha yake yaliisha wiki hii aliposhindwa kuamka kufuatia ukaguzi wa mara kwa mara wa matibabu.

Image caption Ngombe na ibada

Maafisa wanasema kuwa ng'ombe huyo alifariki kutokana na mshtuko wa moyo na matatizo ya mapafu.