Wanajeshi wa Iraq wakaribia Mosul

Wanajeshi wa Iraq wakaribia Mosul baada ya kuwalemea wapiganaji wa Islamic State
Image caption Wanajeshi wa Iraq wakaribia Mosul baada ya kuwalemea wapiganaji wa Islamic State

Jeshi la Iraq na wapiganaji wa kikurdi wanaendelea na mapigano makali kuelekea mji wa Mosul katika harakati za kuwafurusha wapiganaji wa Islamic State kutoka mji huo.

Wapiganaji wa kikurdi tawi la Pesh-merga wamekabiliana vikali na wapiganaji wa IS ili kutwaa vijiji vilivyoko mashariki mwa Mosul huku kukiwa na mashambulio kadhaa ya angani kutoka kwa jeshi la muungano chini ya Marekani viungani mwa mji huo.

IS imejibu mashambulio hayo kwa mashambulio kadhaa ya kujitolea kufa kwa magari yaliyojaa vilipuzi, lakini wanaonekana kulemewa.

Kundi hilo la IS lilitwaa udhibiti wa Mosul miaka miwili iliyopita na limechimba mashimo mengi na mahandaki ya kujificha.