Marubani wasitisha mgomo wao Kenya

Kenya Airways
Image caption Kenya Airways

Marubani katika shirika la ndege nchni Kenya, Kenya Airways wamesitisha mgomo wao uliotarajiwa kufanyika siku ya Jumanne.

Muungano wa marubani umesema kuwa umejiandaa kuipatia serikali muda kutekeleza mahitaji yao.

Mahitaji hayo ni pamoja na kujiuzulu kwa mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo na mwenyekiti wake ambao wanatuhumiwa kushindwa kumaliza hasara,ufisadi na utumizi mbaya wa afisi.