Majeshi ya Iraq yapiga hatua kuishambulia IS

Jeshi la Iraq, likiupigania mji wa Mosul
Image caption Jeshi la Iraq, likiupigania mji wa Mosul

Majeshi ya serikali ya Iraq na Wapiganaji wa Kikurd wamepiga hatua muhimu katika siku yao ya kwanza ya mashambulizi makali dhidi ya kundi la Islamic State katika mji wa Mosul.

Ndege za kivita za Marekani zimeunga mkono kampeni hiyo, iliyoanza jana.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema malengo ya siku ya kwanza yaliyowekwa yalitimia, licha ya kutokea makabiliano ya hapa na pale na wapiganaji hao wenye itikadi kali.

Katika hatua nyingine Umoja wa Mataifa umesema unaharakisha kukamilisha kambi za dharura kwa ajili ya kuwahifadhi raia, ambao wanaweza kuyakimbia makaazi yao kutokana na mapigano.