Riek Machar asema yuko mzima wa afya, Afrika kusini

Riek Machar
Image caption Riek Machar

Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini na Makamu wa Rais aliyetimuliwa Riek Machar aliyesafiri na kuingia Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo yupo Afrika Kusini na kuapa kurejea nyumbani na kusema heshima yake bado ipo pale pale.

Sudan Kusini imekumbwa na mapigano kuanzia mwezi julai na kufunika kabisa makubaliano ya amani yaliyomaliza vita.

Makamu huyo wa zamani wa Rais Riek Machari ametupilia mbali madai kwamba yeye ndiye aliyehamasisha vita.

Miezi mitatu baada ya mashambulizi ya anga na majeshi ya serikali kumlazimisha Kiongozi huyo wa waasi, Riek Machar kukimbia nchi ya Sudan Kusini kutokana na vita ya vya kikabila, ameonekana Afrika Kusini akisema kuwa yu buheri ya afya, wala hajajeruhiwa na kwamba yupo tayari kurejea nyumbani.

Alikuwa akizungumza huku machafuko yakiibuka tena siku chache zilizopita ndani ya taifa hilo lenye utajiri wa mafuta ambapo karibu watu milioni mbii wameyakimbia makazi yao. Riek Machari makamu wa zamani wa Rais amekanusha madai kwamba ni mtu anayependa vita na kwamba ndiye aliyeanzisha machafuko mapya, baada ya makubaliano ya amani yaliyositisha machafuko kwa miaka miwili, kuvunjika mwezi July.

Amesisitiza kuwa majeshi yake yamekuwa yakijihami dhidi ya mashambulizi ya majeshi ya serikali ambapo ameiambia BBC kuwa kundi la waasi bado linaheshimika na linaweza kuleta amani.

Pande zote mbili ambazo zipo katika uhasama mkali zimekuwa zimeshutumiwa kwa kufanya mauaji.

Bwana Machar amerejea msimamo wake wa kujitetea katika mahakama ya kimataifa kama upande wa mahasimu wake nao watalazimishwa kwenda kujitetea.